VITUKO VYA KIAZI
KIAZI
Sehemu ya 1: Shati na Kaptura Mbichi
Kiazi Hataki Shule
Kulikuwa na kijana mmoja wa miaka kumi na nne aliyeitwa Kiazi. Jina hilo hakupewa na wazazi wake. Alilipata mtaani kwa sababu alikuwa na tabia ya kutumia ujanja mwingi kwenye mambo madogo, lakini mwisho wa siku ujanja wake ulimrudia mwenyewe.
Kiazi alikuwa akiishi na bibi yake. Bibi alikuwa mpole, mwenye huruma, lakini akili yake ilikuwa kali kuliko pilipili ya kusaga. Ukimdanganya mara moja, mara ya pili anakusubiri kwenye kona.
Siku moja asubuhi, Kiazi aliamka mapema sana. Si kwa sababu alipenda shule. Alikuwa ameamka kupanga mpango wa kutokwenda shule.
Akiwa anawaza, macho yake yakatua kwenye kaptura yake ya shule. Akatabasamu kama mtu aliyepata jibu la mtihani kabla ya kuingia darasani.
Akaichukua kaptura na Shati, akaenda nayo kwenye ndoo ya maji, akailoweka kabisa. Kisha akaivaa ikiwa bado inachuruzika maji.
Bibi Aingia Mtegoni
Kiazi akaanza kutembea kuelekea jikoni. Kila hatua ilikuwa inatoa sauti: chwaa… chwaa… chwaa…
Bibi alikuwa anachochea uji. Aliposikia maji sakafuni, akageuka kwa haraka.
Kiazi: “Bibi hali ya hewa haikuwa nzuri jana. Nilifua lakini haikukauka. Hakuna shida, mbona inavalika tu.”
Bibi akamwangalia vizuri. Kaptura ilikuwa imemkaa kama mtu aliyekaa kwenye beseni.
Kiazi: “Bibi usinizuie. Elimu ni muhimu. Mimi lazima niende shule.”
Alisema hivyo huku akitembea kuelekea mlangoni polepole sana, akitamani bibi amzuie kwa nguvu.
Bibi akamshika mkono. Kiazi akaanza kulia kilio cha kiufundi.
Bibi akamhurumia. Akampa uji akae karibu na jiko apate joto. Kiazi akanywa uji kwa raha mpaka akauliza:
Hapo bibi akajua kuna mchezo.
Mtego Warudi Kwa Kiazi
Bibi hakubishana naye. Aliingia chumbani, akarudi na kitenge kikubwa.
Kiazi: “Kazi gani tena bibi?”
Kiazi akameza mate. Mpango wa kupumzika ukageuka kuwa kazi ya siku nzima.
Kiazi Aumbuka Mtaani
Baadaye Kiazi alitoka nje kufagia akiwa amevaa kitenge. Watoto wa mtaa walipomwona, wakaanza kucheka.
Kiazi akajifanya hajali.
Lakini moyoni alijua kabisa kuwa amejifunga mwenyewe. Alikwepa shule, lakini akakutana na kazi ngumu kuliko hesabu.
Siku hiyo Kiazi alijifunza jambo moja: wakati mwingine ukikimbia darasa, unaweza kuishia kusoma maisha kwa viboko vya kazi.
Soma Kisa Kinachofuata
Kiazi anakuja na ujanja mpya wa kukwepa shule. Safari hii anajipaka dawa ya meno usoni na kudai amepata “ugonjwa wa kusoma sana”.
SOMA KISA KINACHOFUATA →
Maoni ya Wasomaji
Maoni yataonekana hapa kama comments zimewashwa kwenye post hii.
Andika Comment