JICHO LA USALITI

Jicho la Usaliti - Ndoto

SEHEMU YA TATU

SURA YA TATU

Tuliandaa sherehe kubwa sana pale nyumbani, baada ya kuchukua pesa benki, ilikuwa ni siku yenye furaha pasipo kifani, nilimkumbatia mdogo wangu Jane kuonesha ishara ya upendo kama mlezi niliyebaki, ilipofika saa 4 usiku kila mtu aliyenda kulala kwa makubaliano asubuhi tutafanya kikao cha kugawana pesa.

Wakati nimelala niliota ndoto mbaya sana, niliota nimekufa na nipo mbinguni, akaja malaika mbele yangu nakuniambia kwamba nimetolewa roho yangu kwa bahati mbaya hivyo nitarudi duniani kama kuku, gafla nikajikuta nipo ndani ya kibanda cha kuku huku nikipata hisia nisiyo ifahamu, kuangalia pembeni yangu nikaona jogoo kubwa sana nikaliuliza,

Ian: ni hisia gani hii,

Jogoo: ushawahi kutaga yai wewe?

Ian: hapana sijawahi,

Jogoo: hilo ni yai linataka kutoka wewe, hivyo kamua kwa nguvu,

Nikakamua mara ya kwanza, likatoka yai, nikaendelea kukamua tena na tena yakatoka mayai mengi tu, ghafla nikasikia.

Edwin: we jamaa! Mbona unajisaidia kitandani?

Niliamka haraka nikaona kweli nimeharibu kitanda chote, niliona aibu sana, nikakimbia bafuni na mashuka kisha nikafua na kuoga, niliporudi nikamuomba Edwin asiwaambie Jane na Robert, akaniahidi kwa kiapo kwamba hato waambia.

Ilipofika asubuhi, kama kawaida tulijiandaa tukapata kifungua kinywa, siku hii vitafunwa vilikuwa vizuri sana kutokana na mfuko kutuna, tulifurahi sana, wakati tukinywa tulitaniana na kufanya chai kuwa tamu zaidi. Baada ya chai tukakaa ofisini na kuanza kikao cha kugawana mapato.

Ian: sasa jamani fedha tuliyopata ni shilingi milioni 35,

Jane: hapana kaka ni milioni arobaini,

Ian: hela tuliyopata ni milioni 35, iyo milioni 5 nimepewa binafsi kama zawadi inamaana hamkusikia alivo niambia?

Edwin: lakini kaka, mbona hata Robert amejitolea hii nyumba bila kutaka malipo yeyote, kwanini na wewe ukaacha fedha zote tukazi gawanya kwa wote sawa!

Jane: kweli kabisa, ujue sisi ni ndugu hatuna budi kuanza kuwekeana matabaka kama kipato tumekipata ni bora tugawane wote sawa, nakuomba kaka ugawe sawa kwa wote.

Ian: hivi mnajua maana ya mtu kupewa zawadi? Mbona mnakuwa mamburura nyinyi, kwanza hata majukumu ukiangalia mimi ndio nimefanya kazi sana acheni hizo bwana,

Jane: kaka unakosea kwa kweli, wote tumefanya kazi ngumu na sisi sote kama kwenda mahakamani tutahukumiwa kesi moja ya utapeli, hebu kuwa muungwana kaka angu ili tusonge mbele kwa mtindo huu, hatuta songa mbele,

Ian: Jane nitakupiga kofi unanisikia wewe, mbona unaakili tatu na nusu wewe!

Edwin: jamani! Jamani! Jamani! Naomba yaishe, tufanye yaliyo tuleta, igawanywe hiyohiyo milioni 35.

Robert: mh! Sawa

Tulianza kugawana fedha ambapo kila mtu alipata milioni 8 pointi 75, baada ya kugawana tuliagana kisha mimi na Jane tukaondoka na kwenda nyumbani kwetu, kwa nia ya kukarabati nyumba na kuendelea na maisha, lakini tulikubaliana tutakutana tena wote wanne baada ya mwezi na nusu ili kuendeleza kanisa letu.

Baada ya mwezi mmoja na nusu, mimi na dada Jane tulifunga safari hadi nyumbani kwa kina Robert, tulipofika tulikuta nyumba imeuzwa na inaishi familia nyingine mpya, baada ya ku wadadisi wenyeji wakatuambia kijana mwenye ile nyumba amewauzia na yeye amekwenda kuishi mji mkuu, niliumia sana kwani hata simu zao ni wiki ya pili hazipatikani, tulishikana mikono na dada tukarudi nyumbani kwetu kwa shingo upande.

Baada ya wiki moja nikiwa nimekaa sebuleni na Jane tuliona tangazo kwenye televisheni ya taifa tangazo likiwaalika watu kwenda kusali katika kanisa liitwalo KANISA LA WAGAWANAO SAWA, na anaoneka Robert na Edwin ndo wachungaji wakuu, nikagundua kumbe wameenda kuanzisha kanisa lao jipya, nikakosa nguvu kabisa, Jane akaniambia,

Jane: Kwa uelewa wangu mdogo nilihisi tu haya kuja kutokea, hata si shangai kaka yangu, utengano mwingi hutokea sio kwa sababu ya kujenga bali ni kwa kutofautiana kimasirahi, alafu kaka yangu ngoja nikwambie hebu tuachane na hii kazi ujue tuna mzingizia Mungu ata kuja kutupa mapigo matakatifu, hebu kumbuka tu ndoto yako ile?

Ian: ndoto gani?

Jane: ndoto gani? We umesahau ulifanya nini kitandani,

Ian: oooh! Jamani mimi, mbona Edwini alini ahidi hatowaambia kamwe!

Jane: hata sisi alituambia vivyo hivyo, tusikwambie hahaha dunia nzuri sana hii tatizo wanadamu magumashi mengi,

Niliona aibu sana kusikia hivyo, nikamsihi dada twende kwa Bosi tukakiri makosa yetu.

Tulipofika tukamkuta Bosi, alitukalibisha kwa furaha sana yeye na mke wake, nikamueleza ukweli tupu, Bosi alicheka sana akasema hana tatizo na mimi kwani anafuraha kuwa na familia yake, na kikubwa zaidi tangu ameacha tabia za rushwa amepandishwa cheo zaidi na kupata marafiki wenye tija wengi sana, tulishikana mikono na kukumbatiana kisha tukaimba wimbo wa kumsifu Mungu, ilipofika jioni mimi na dada Jane tulirudi kwetu kwa furaha na amani tele.

Umeipenda makala hii? Washirikishe wengine kupitia WhatsApp.

Share WhatsApp

Maoni ya Wasomaji

Maoni yataonekana hapa kama comments zimewashwa kwenye post hii.

Andika Comment