FITINA ZA BIASHARA-SURA YA 2
Fitina za Washindani
Jifunze kuziona kabla hazijakufikia.
Washindani wote si maadui zako. Wengi wao wanakufanya ubunifu zaidi, wakikupa sababu ya kuboresha huduma zako kila siku. Lakini wapo wachache ambao hawaamini ushindani wa haki. Kwao, njia rahisi ya kushinda si kuboresha biashara yao bali kuiharibu yako.
Fitina nyingi huanza pale biashara yako inapoanza kupata jina. Ukiwa mdogo hakuna anayekujali. Lakini ukianza kupata wateja wengi, hapo ndipo macho mengi huanza kukuangalia.
Fitina ya Kwanza: Kuharibu Sifa
Hii ndiyo silaha inayotumiwa sana duniani. Mteja akipoteza imani, hata bidhaa bora inaweza kukosa soko.
Wapo watu watakaosambaza taarifa kuwa bidhaa zako ni feki, kampuni yako imefilisika, unatapeli wateja au huduma zako ni mbovu. Mara nyingi hawana ushahidi wowote, lakini wanajua kuwa habari mbaya husambaa haraka kuliko ukweli.
- Jibu malalamiko ya wateja kwa haraka.
- Jenga brand yenye uaminifu.
- Kusanya ushuhuda wa wateja halisi.
- Usigombane mtandaoni.
- Ruhusu kazi yako ijitetee.
Fitina ya Pili: Kuiba Wafanyakazi Muhimu
Mshindani anaweza asikununue biashara yako, lakini anaweza kumnunua mtu anayejua siri zote za biashara yako.
Mfanyakazi anayejua supplier, bei zako, mfumo wa mauzo na wateja wako ni mali kubwa kuliko mashine nyingi.
• Wafanyakazi wasijue kila kitu.
• Gawanya majukumu.
• Linda taarifa muhimu.
• Tengeneza mazingira mazuri ya kazi.
Fitina ya Tatu: Kushusha Bei kwa Hasara
Makampuni makubwa wakati mwingine huuza chini ya gharama kwa muda mfupi ili biashara ndogo zifunge.
Baada ya washindani kuondoka sokoni, wao hupandisha tena bei.
Shindana kwa ubora wa huduma, uaminifu, kasi ya huduma na uzoefu wa mteja.
Fitina ya Nne: Kuiga Chapa
Baadhi ya watu hutengeneza bidhaa zenye nembo inayofanana na yako. Wateja wakinunua bidhaa hizo wakidhani ni zako, sifa yako huanza kuharibika bila kosa lako.
Sajili nembo yako mapema na hakikisha wateja wanajua namna ya kutambua bidhaa halisi.
Fitina ya Tano: Fake Reviews
Katika dunia ya leo, watu wengi hununua baada ya kusoma maoni ya wengine.
Washindani wanaweza kulipa watu wasiowahi kutumia huduma yako waandike maoni mabaya ili kuwazuia wateja wapya.
Omba wateja wako halisi waache maoni ya kweli.
Usinunue reviews.
Ukweli hudumu kuliko uongo.
Hizi ni baadhi tu ya mbinu zinazotumiwa na washindani. Kadiri biashara inavyokua, ndivyo mbinu hizi zinavyobadilika. Lakini kuna eneo moja ambalo ni hatari zaidi kuliko washindani wote. Ni pale adui anapotokea ndani ya kampuni yako mwenyewe.