JICHO LA USALITI SEHEMU YA KWANZA
SEHEMU YA KWANZA
SURA YA KWANZA
Ilikuwa ni siku ya jumapili ya pata saa 2:45 asubuhi, anga la bluu, ndege wa kirukaruka angani na kutua katika matawi ya miti na maua kana kwamba wanafurahia uzuri wa mimea na rangi tofauti tofauti za maua yanayo nukia harufu tamu. Njiani wanaonekana wapita njia wakiwa nadhifu kwa mavazi waliyo ya vaa na mikononi wameshikilia biblia zinazo toa tafsiri sahihi kwamba walikuwa wakienda katika nyumba zao za ibada.
Wakati huo mimi na mdogo wangu Jane tulikuwa tume mzunguka mama yetu mpenzi alie lala kitandani akisumbuliwa na ugonjwa, tulikuwa tupo katika shauku kubwa ya kutaka kujua mama yetu kipenzi na furaha ya moyo wetu ana sumbuliwa na ugonjwa gani.
Baada ya muda mfupi daktari alifika wodini nakuanza kuzungumza na mama.
Daktari: habari za asubuhi,
Mama: salama dokta
Mimi Na Jane: shkamoo dokta
Daktari: Marahaba watoto wazuri, naomba mwende nje kidogo ni ongee na mama sawa?
Mimi Na Jane: (kwa pamoja) sawa daktari
Baada ya sisi kuondoka daktari akaanza kuongea na mama.
Daktari: Mama unatatizo la saratani ya shingo ya kizazi, ambalo limesababishwa na virusi vinavyo itwa Human papilloma (HPV).
Mama: ooh! Mungu wangu
Dokta: kinga yako ya mwili ilishindwa kuondoa hayo maambukizi, chembe hai za kawaida zikaanza kukua bila mpangilio na kusababisha dalili za awali za saratani, lakini nasikitika hukuzijua dalili hizo mapema.
Mama: ooh, kwaiyo ndio nimeisha kufa tayari babaangu?
Daktari: hapana mama tutajitahidi kukuhudumia vizuri, usipate hofu.
Mama: Mungu wangu nisaidie mimi!
Daktari: kuna njia tatu ambazo hapa hospitali tuna zimudu njia ya kwanza ni Trachelectomy hapa manaake tunaitoa shingo ya kizazi nakubakiza mfuko wa uzazi kwa ajili ya uzazi hapo siku za baadaye. Njia ya pili ni Radiotherapy tuna tumia mionzi kutibu saratani iliyosambaa, na tatu ni chemotherapy hii ni njia ya dawa za vidonge na sindano. Kwahiyo mama hapo ni wewe tu kuchagua njia ambayo unaona kwako ni naafuu.
Mama: bora vidonge na sindano daktari
Daktari: Sawa mama, kwa sasa tunaupungufu wa dawa hizo, na pia wataalamu wa njia zingine nao tuna waazima toka hospitali ya mtakatifu George, hivyo matibabu tutaanza rasmi kesho kutwa, sasa hivi utahamia katika chumba maalumu kwa ajili ya uangalizi ukisubiri siku ifike.
Mama: sawa daktari nimekuelewa,
CHUMBA MAALUMU - JIONI
Kama kawaida yetu Mimi na mdogo wangu Jane tulikuwa tupo na mama tukimzunguka na ku mfariji taratibu, muda huu mama kwa huzuni alikuwa akituangalia kwa macho makini sana kana kwamba anatafakari jambo fulani, akaniita.
Mama: Ian mwanangu
Ian: ndio mama
Mama: (kwa sauti ya masikitiko) Tangu Baba yenu afariki dunia miaka miwili iliyo pita kwa kupigwa risasi na bosi wake ili tu asimlipe madai yake, koh...Koh...koh, mimi nimekuwa ndiye mlezi pekee niliye baki, sindio mwanangu?
Ian: ndio mama!
Mama: basi kuanzia sasa wewe ndio mlezi mpya wa dada yako.
Jane: mamaaaa! Kwanini unasema hivyo?
Mama: mh! Jane mwanangu kua uyaone.
Baada ya kusema hayo mama alimtazama Jane akamshika mashavuni na mikono yake miwili, kisha akatoa tabasamu hafifu lililo jaa upendo mkubwa. Muda wote huo nilikuwa nikitoa machozi kimyakimya huku nikimtazama mama bila kupata majibu ya swali langu kwamba naota au ni kweli ninayo ya sikia.
Mama: Jane binti yangu
Jane: ndio mama angu!
Mama: kimbia dukani Kwa mzee kibotro kaninunulie maziwa ya maji nahisi njaa
Jane: sawa mama
Baada ya Jane kuondoka tu, mama alinitazama usoni bila ku kwepesha macho Kwa sekunde kadhaa, kisha akasema
Mama: Ian mwanangu, una miaka 17 sasa ushakuwa mkubwa, hata kama wenzako wa umri huo bado wanakuwa chini ya uangalizi wa wazazi wao, lakini siku zote matatizo huleta uzoefu ambao ni faida katika jamii na pia tambua vidole havi lingani
Ian: ndio mama najitambua
Baada yakusema hivyo nili jipangusa pua iliyo kuwa iki vuja majimaji kama vile chemchem kutoka mlima Kilimanjaro.
Mama: Dada yako Jane bado mdogo ingawa ana akili Sana za kuzaliwa, lakini miaka yake ni 12 tu hivyo anahitaji uangalizi wakaribuu Kama…………
Ian: Kama nini? Kama nini mama? Mbona unaongea kama mtu anaye aga, una mpango wa kwenda sehemu kuugulia mama? mbona daktari kasema uvute subira wakija hao wataalamu utapata matibabu na utapona kabisa.
Niliongea kwa uchungu sana huku niki lia kama mtoto mdogo wa miaka 5
Mama: Ian mwanangu, mtu yeyote Yule, haidhuru awe mbali vipi na shughuli za kisayansi, mapambano ya kisiasa, harakati za kimapinduzi, na kadhalika, huwa na hamu ya kutaka kujua vile ulimwengu utakavyo kuwa kwa wakati ujao.
Akatulia kidogo kisha akaendelea
Mama: mwanangu mpenzi
Ian: ndio mama!
Mama: malimwengu ya mzungukayo mwanadamu hayana kikomo wala mipaka yoyote ile na hatimaye kujaa siri ambazo mwanadamu anaweza kuzigundua kwa taratibu tu, hatua kwa hatua, lakini hatafaulu kamwe kuzijua zote kwa ukamilifu.
Akanitazama usoni kidogo kisha akasema kwa upole,
Mama: Ninyweshe maji kidogo mwanangu
Nikachukua maji kwenye jagi lililo kuwako pembeni yangu nika mimina robo katika kikombe ki kuukuu naku mnywesha, baada ya kunywa fundo moja aka kohoa kivivu kisha akaendelea kuongea.
Mama: kifo……….
Nika shtuka baada ya kusikia kasema hivyo nika mshika mkono wake, aka endelea.
Mama: kifo hakihitaji kumsumbua mtu yeyote Yule kwa sababu ni Yule tu anayeishi ana hisia ama za maumivu au furaha. Hivyo basi nitakapo pumzika sitapata mateso haya makali ya mwili, naomba umtunze mdogo wako.
Baada ya kusema hayo ali jinyoosha akakata roho. (kimya)
Nakumbuka lilikuwa nitukio gumu sana hasa pale Jane aliporudi na maziwa yaliyo kosa mtumiaji, jinsi alivyo lia na kuomboleza kwa uchungu zaidi ya mtu anaechomwa na mto, niliumia sana moyoni, lakini na mshukuru Mungu kwa msaada wa ndugu na marafiki wa mama waliofika baada ya mama kufariki, tuliweza kumlaza mama yetu katika nyumba yake milele.
Baada ya mwezi mmoja nilifanikiwa kurudi shuleni kumalizia kidato cha nne, kaka yake mama aitwaye Mwagito alichukua jumu la kunilipia mahitaji ya shule pamoja na hostel, Jane pia alimchukua nyumbani kwake.
Maoni ya Wasomaji
Maoni yataonekana hapa kama comments zimewashwa kwenye post hii.
Andika Comment