JICHO LA USALITI
SURA YA PILI
Tulikuwa tukitembea tembea na rafiki yangu Edwin, tukitazama makundi mbalimbali ya wanafunzi, wengine wakicheza basketball, football na wengine netball, tukiwa tunaelekea kwenye upande wanakocheza netball Edwin alikuwa akinitania.
Edwin: Aah! Kaka siku ya msiba wa mama ulikuwa unalia kama marehemu bibi yangu, akiwa na njaa.
Ian: Wee dogo acha masihara kwenye mambo mazito, unakuwa kama pimbi bwana.
Edwin: Hahahaha kuna muda ulipandisha geji hadi ukaingia kaburini, ila yule mlevi alipokutupia spedi moja ya mchanga kichwani ulitoka haraka kama paka.
Ian: We bwana we! Kaburi achana nalo, hata wale watu wazamani waliokuwa wanapakata maiti ya chifu kisha wanazikwa nayo wakiwa hai, lazima walikuwa wanapiga pombe au bange kwanza.
Wote: Hahahahahahahahahaha.
Edwin: Unavotoka kaburini ulipiga yowe! Upo, natania, natania jamani uwiiii, ukatoka haraka hatari hahahaha.
Ian: Hahaha we boya kweli, badala ya kuhuzunika na mimi, wewe kazi yako kupiga mimacho tu wanayo fanya watu, pumbavuuuu.
Edwin: Jokes bana! Daah kaka cheki watoto wa netball hao, vivazi hivyo sasa nafwaaa jamani mie mtoto wa binadamu mwenzao.
Ian: Unajua nini mwana, tukakae engo ileee pale, alafu tukifika tunalala chini ili tuone vizuri kazi ya muumbaji.
Wote: Hahahahaha (tukagonga).
Tulipofika engo ile tukalala chini kwenye nyasi ili tuone vyema maana nguo wanazo vaa wacheza netball tabu tupu, na sisi ndio ujana unatusumbua tutafanyaje sasa kwa mfano.
Tukiwa tumelala pale tukaendelea kupiga soga.
Edwin: Fuuu, fuuu... (anapuliza na mdomo akidhani atavifunua visketi zaidi).
Ian: Hahahaha! Kaka umechoka kweli kiakili na kimwili, sasa kwa umbali huu unadhani utawafunua zaidi? Apo sali sana upepo tu uje wakutosha.
Mungu si Athumani, upepo mwororo ukanisikia nimeutaja, ukaanza kupuliza taratibu kama umeelekezwa cha kufanya vile.
Edwin: Ooooh! Oooh! Upepo shikamoo, loooh! Kumbe wanacheza walimu na wanafunzi.
Ian: Ndiyo! Ulikuwa hujajua, mcheki Madam Chinda yuleee.
Edwin: Ayaaah, hahaha duu maticha wangepewa nguo ndefu kidogo, mh kumbe ana kitumbo vile, ila mguu ule hauzeeki aseeh!
Ian: Pwaaaa!
Nikampiga mbata shingoni.
Ian: Panyabuku wewe acha kumsema mwalimu wangu, afu yule ni sawa na mama yako tu.
Edwin: Mama yake nani? Nenda nyumbani kwenye kabati kachukue kadi langu la kliniki uone kama kimendikwa jina lake mle, alaaah!
Ian: Sasa unalilia nini? Si kiheshima wewe.
Edwin: Toka bwana, acha mi ni concentrate kwenye somo langu hapa takatifu la chabo.
Ian: Mh! Ingekuwa darasani hapo ungekuwa ushasinzia muda mrefu.
Edwin: Ndiyooo! Darasani fani na maudhui haviendi pamoja. Sa ntafurahije? Cheki hapa yani fani na maudhui sambamba kabisa hadi mtu huchoki kula pindi.
Wakati tumetingwa na kutazama wanaocheza netball, mwalimu wa nidhamu alikuwa anatufatilia kitambo mchezo wetu.
Edwin naye kaingiza mkono ndani ya suruali anajishika kwenye kipaza sauti chake huku uso wake ukiwa umeelemewa na mchezo wa kijinga.
Ghafla mwalimu akatunyemelea taratibu mpaka nyuma yetu, akamchapa Edwin fimbo moja ya nguvu matakoni.
Vuuuuup!
Tulishtuka sana tukasimama haraka. Wakati na mimi nainuka akanipiga kibao cha nguvu.
Pwaaaaah!
Nikapepesuka kama mlevi.
Nilipopata usawa haraka nikaungana na Edwin kukimbia mpaka nyuma ya madarasa. Tukatafuta sehemu tukakaa chini huku tunahema kwa nguvu sababu ya kukimbia na mshituko pia.
Edwin: Duuh! Ticha kanichapa katikati ya mgongo na tako, mwee! Walimu wengine bwana, kufundisha hawajui ila kwenye kuchapa nawapa A.
Ian: Pole sana, hivi hapo huwezi kuzaa milele kwa kile kichapo?
Edwin: Tangu lini mwanaume akazaa! Pua yako.
Ian: Siyo hivyo, yaani namaanisha huwezi kumpa mwanamke ujauzito.
Edwin: Ahaaa! Hapo sawa, haina shida sitampa, nitamkopesha au nitamwazima tu.
Ian: Mwee, kichwa hiki boga kabisa! Pole kwa serikali inayopoteza hela zake kusaidia mambururaaa.
Wakati tumekaa bado nyuma ya shule tuliwaona wanafunzi wakike watatu wakimsongasonga mvulana na kumsonyoa sonyoa kana kwamba wanataka kumpiga.
Walisikika wakisema:
Wasichana: “Ooh we mwanaume feki, tena baba la wanafiki! Kazi kufuatilia mambo yasiyokuhusu, tutakuvalisha kanga.”
Tulisogea haraka katika eneo la tukio.
Ian: Jamani, tunaomba msameheni mdogo wangu huyu, ni utoto tu unaomsumbua. Akikua ataacha.
Msichana wa 1: Hakuna bwanaa, amezidi huyu mdogo wako. Yaani haishi kutufuatilia mambo yetu.
Msichana wa 2: Ntamuua huyu alafu nimtupie jalalani mimi.
Edwin: Alafu! Ukishamtupa jalalani usiku unarudi kumuokota anakuwa wa kwako wote wote si ndiyo?
Msichana wa 2: Kaka najiheshimu eeh! Afu mi sitembei na vichoko kama hivi upo?
Edwin: Heheheeee warere, ila we kweli maana hapo tu una miaka 16 lakini ushambeba mheshimiwa diwani. Kitu kina miaka 60 kudadeki na ukakimudu, daa we ni kwikwi aseeh!
Wasichana wote: Hehehehe, yashakuwa hayo!
Wakafyonya kisha wakaondoka kwa aibu sana huku wakionekana wakiteta jambo.
Ian: Mwanangu Edwin we mpana! Umejuaje ishu za yule dada maana kalowana hatariii.
Edwin: Mimi kifaru cha Somalia dogo, ohoooo.
Ian: Hahaha umetisha kama njaa kaka. Enhee na wewe Robert, ilikuwaje mpaka yanatokea haya? Unatutilia aibu wanaume wenzako.
Robert: Ujue nini bro, mi napenda sana kufuatilia watu. Yaani ndo raha yangu, ila wala mi siyo mnoko.
Edwin: Pumbavuu! Haya njoo nyuma yangu unifuatilie na mimi. Twendeee.
Ian: Bwana eeh, nyamaza uko na falsafa zako za chooni. Nimemuuliza Robert sio wewe.
Edwin: Sawa spika wa bunge, naomba kutoa hoja!
Ian: Tokaaa! Sasa Robert, baada ya prepo tuonane hostel sawa? Uje room kwetu nitakupa mchongo dogo.
Robert: Sawa bro. Nashukuru sana kuniokoa, maana leo ningeumbuka. Ningepigwa si mchezo.
Ian: Hahahaha poa poa Robert. Baadaye usisahau kufika.
Robert: Poa kaka.
Huku akiondoka.
Ian: Ujue nini kaka, nina bonge la idea aseeh.
Edwin: Lipi hilo kaka?
Ian: Usijali, nitakupa mchongo mzima tukiwa hosteli kabla Robert hajaja.
Edwin: Poa jembe.
BWENINI – SAA 4:30 USIKU
Kinaonekana kitanda dabo deka. Juu hakuna mtu ila kitanda cha chini tumekaa mimi na Edwin na miguu haigusi chini, migongo imeegama ukutani.
Tukawa tunaongea taratibu sana ili tusiwaamshe waliolala.
Ian: Ujue nini Edwin, mi nataka tufungue kanisa kaka, unaonaje?
Edwin: (Kwa mshangao mkubwa) We jamaa! Umeanza kutaga nini? Mawazo gani hayo?
Ian: Kaka sio ivo!
Edwin: Sio ivo nini? Hapo ulipo mdhambi shetani haoni ndani. Halafu mimi macho yangu tu yamekaa kiwiziwizi, nani atakuwa pasta? Labda niwe mhasibu.
Ian: Hahaha Edwin bwana! Ni hivi, hili kanisa litakuwa la kipekee. Mfumo mpya hapa mjini. Lenyewe litakuwa ni kanisa huria, upo?
Edwin: Nipo ndiyo! Ina maana hunioni hapa?
Ian: Unajua nini Edwin?
Nikamnong’oneza mpango mzima sikioni ili watu wasije wakasikia.
Edwin: Hahaha!
Akashuka chini kwa furaha huku akiongea kwa nguvu sana.
Edwin: This mother fucker did it! Hahaha! He did it meeeen!
Mwanafunzi: Oya acha kelele watu tumelala bwana.
Edwin: Acha kuzingua bwanaa. Kwenu kitanda cha kamba nini hadi uje kulala hapa?
Mwanafunzi: Edwin nitakubonda wewe!
Ian: Kaka we lala bwana. Hujamzoea tu huyu, kichwa chake cha panzi.
Alipolala yule mwanafunzi, Robert naye akaja. Tukakaa mimi, Edwin na Robert kwa sauti ya chini sana tukapanga mikakati yetu.
Baada ya muda kupita wote tulimaliza shule na kurudi makwetu.
NYUMBANI – ASUBUHI
Inaonekana nyumba ya wastani, ni nzuri kiasi. Chumbani kunaonekana kitanda kibovu cha futi 5 kwa 6, meza ndogo kuukuu na kabati la nguo. Chumba kingine ni ofisi ambayo tumeitengeneza kwa kuweka vifaa pamoja na meza zetu.
Edwin: Hivi Robert, wazazi wako walipofariki hii nyumba ndiyo walikuachia urithi?
Robert: Ndiyo kaka.
Alijibu huku akiendelea kupanga nguo kwenye kabati.
Edwin: Ok, ok... itabidi nikudhulumu.
Ian: Mh!
Robert: Unaota mchana bro!
Edwin: Yaaah, kwani hunioni navyo koroma hapa? Aisee kumbe. Sasa unaishije, chakula na mahitaji mengine? Maana umezaliwa peke yako na huna ndugu wa undugu kufaana.
Ian: Huku nikiwa nimelala chali kitandani, nikasema:
Ian: Kaka utadhani mgambo hayo maswali. Yaani wewe mchungaji pyuaaa kabisa.
Edwin: Nyoo! Hebu tulia wewe.
Robert: Hahaha.
Ian: Tena now patakuwa makao makuu ya Kanisa Huria la nchi hii.
Wote: Hahahahaha!
Kisha tukagonga.
Edwin: Mungu atusamehe sana.
Niliinuka kitandani nikamsogelea pale mezani alipokuwa. Wakati nafanya hivyo akaacha kuunganisha kompyuta na vifaa vyake na kunitazama kwa tahadhari kubwa sana.
Nikaongea huku nikimtazama usoni kiume.
Ian: Kwanjia zetu kuu tano za ufahamu, tunapata taarifa mbalimbali tofauti kuhusu kitu kilekile kwa nyakati tofauti na chini ya mazingira tofauti.
Muda huu Robert akaacha kupanga nguo kabatini na kunisikiliza kwa makini.
Alipoona namtazama akashtuka kidogo kisha akaendelea tena kupanga, lakini masikio yake yote yakawa kwangu.
Edwin naye alikuwa akisikiliza kwa nidhamu na butwaa kubwa.
Niliendelea kuongea huku nikitembea tembea mle chumbani na mikono yangu ikishiriki mazungumzo kwa vitendo.
Ian: Tazama Wakatoliki mwaka 1054, chini ya utawala wa Papa Leo III ulitokea utengano ambapo kukatokea Eastern Orthodox. Mwaka 1517 Martin Luther kutoka Ujerumani akaanzisha pia dhehebu la Walutheri. John Calvin na John Knox mwaka 1500 na 1560 wakaanzisha Wapresbiteri, na baadaye kukaendelea kuibuka madhehebu mapya lukuki.
Edwin alikuwa akinisikiliza kwa makini sana. Robert naye uzalendo ukamshinda akaacha kabisa kupanga nguo na kubaki akinitazama na kunisikiliza kwa makini.
Ian: Edwin! Robert! Hebu tazama kutoka mbali kwa mfano, nyumba ya mraba huonekana duara. Mandhari huonekana tofauti katika nyakati tofauti za mchana. Na kwa watu wengine asali ni chungu wakati kwa wengine ni tamu.
Hivyo basi binadamu tupo katika kusaliti tu na sio kujenga palipo na udhaifu. Kama nia ni kuboresha, hakukuwa na haja ya wazee wetu kujitenga. Iliwapasa hata wafe wakipigania kufanya maboresho.
Lakini wao waliamua kuanzisha vyama vya siasa vipya, makanisa mapya na wengine kuoa wake au kuolewa upya. Yote ni sababu ya maslahi binafsi.
Ona! Mama Afrika mpaka leo anashindwa kuwa taifa moja chini ya rais mmoja kwa sababu tu ya usaliti na uroho wa madaraka.
Vipi kuhusu sisi iwe shida kuanzisha kanisa letu?
Acha tu tuendeleze madhambi haya.
Edwin na Robert walitabasamu kwa mshangao mkubwa kisha wakanikumbatia.
Robert pia alisogea na kunipa mkono.
Ian: Sasa basi kanisa letu litakuwa na idara kuu nne.
- Idara ya kwanza ni Mipango na Utekelezaji, itakuwa chini yangu.
- Idara ya pili ni Teknolojia, Edwin utasimamia.
- Idara ya tatu ni Upelelezi, itaongozwa na Robert.
- Idara ya mwisho ni Uhasibu, itasimamiwa na Jane ambaye atafika baadaye jioni.
Robert: Katika kitengo hiki cha upelelezi naruhusiwa kuwa na wasaidizi wa muda?
Ian: Yah! Lakini wakipata data unazohitaji wakukabidhi, wape chao wachape lapa. Si vema wakafika hapa. The same to you Robert.
Ilichukua muda kupanga mikakati yetu. Ilipofika jioni dada Jane aliwasili.
Alionekana akigonga hodi mlangoni.
Jane: Ngongongongo!
Robert: Karibu.
Alipofungua alitoa tabasamu lakini alihisi kwamba ni Jane ila hakuwa na uhakika kwa sababu hawakuwa wakifahamiana.
Jane akaingia ndani.
Edwin na Ian: Waooooooh!
Tukaenda kumkumbatia kwa furaha.
Edwin: Nambie mhasibu pasipo fani.
Jane: Poapoa IT wa maboksi upo.
Ian: Hahahahaha, watani wa jadi.
Baada ya muda tuliandaa mpango mzima wa kazi kwa ajili ya kuanza rasmi.
Maoni ya Wasomaji
Maoni yataonekana hapa kama comments zimewashwa kwenye post hii.
Andika Comment