NYUMBANI - JIONI

SEHEMU YA PILI

NYUMBANI – JIONI

Ukutani kwenye notice board zinaonekana picha za kigogo wa serikali zikiwa zimepigwa katika maeneo tofauti tofauti na zimebanwa na pini, muda huu kila mtu yupo makini na kazi yake, Edwin anaonekana akiunganisha nyaya na vifaa vingine kwenye kompyuta 3 zinazofanana, baada ya kumaliza anapukuta kiti chake vumbi kisha anakaa, akageuka upande wake wakushoto akachukua miwani yake kutoka kwenye begi akaivaa, akaendelea na kubofyabofya kompyuta zake kwa ustadi mkubwa huku akila bisi (pop corn)

Edwin: (Kwa mshtuko) damn it! Nimefanikiwa kuiba wireless ya muhindi apo jirani

Jane: ooooh! Wayalesi sasa yanini? au unataka uanikie nguo, mi nikajua umefanikiwa kutengeneza ATM mashine watu tupige mapesa maana umeongea kwa mshtuko sana

Mimi na Robert tukatazamana tu kisha tukacheka

Ian: hongera sana Edwin, lakini leo mmekutana maboga mawili sijui nani ata msaidia mwenzake,

Robert: haswaaa!

Jane: Kama mi boga sichana basi na wewe boga vulana, haiwezekani mi nikawa boga alafu wewe ukawa mtu never.

Ian: hahaha fasihi imekupitia matakoni dogo

Jane: (akashituka) iko wapi kaka! (Akasimama anaiangalia iyo fasihi nyuma ya kiti)

Ian, Edwin, Robert: hahahahahaha

Jane: mnacheka nini sasa, nitawapiga ohooo! Na mu iambie iyo fasihi hata siiogopi na nita ipiga kichwa kama mpira wakona vile, mimi ni hatari!

Aka simama juu ya kiti chake, akainua mikono uku kakunja ngumi, akawa ana tuonesha misuli ya mikononi,

Jane: mnaona? (Huku anakunja shati tuone misuli yake membamba) misuli hii minaweza kubeba jaba la lita ishirini

Edwin: bila maji sawa!

Jane: bila maji? Muone sura yake kama ikulu ya nyani

Ian: kaa chini dada angu mpenzi endelea na mahesabu, maana we ni profesa wa uhasibu bila hata kungia darasani, kweli pesa noumaa!

Nikamsogelea kwenye meza yake nikamsaidia aka kaa chini, nilitupia jicho kwenye makaratasi yake nikaona kachora jedwali lenye tarehe, maelezo ya pesa, pesa zinazoingia, pesa zinazotoka, akiba. Nilifarijika sana kuona anafanya kazi nzuri, pamoja na umri na elimu ndogo.

Edwin: Robert hebu sogea hapa kwangu

Robert anaacha kuweka alama za michoro kwenye picha zilizo bandikwa kwenye notice board ana msogelea Edwin

Edwin: nimefanikiwa kupata mazungumzo ya Yule kigogo wa serikali, sasa toa laini yako unipe ili tuonganishe, uwe unapata kila simu na meseji zake.

Robert akarudi mezani kwake nakuchukua simu yake haraka, nakumkabidhi Edwin, Edwin alipokea na kuitoa laini kisha akachomeka kwenye kifaa kama kiboksi cha kibiriti nakuanza kuonganisha kwa umakini mkubwa, baada ya dakika kadhaa akaitoa na kumpa Robert aiweke kwenye simu yake tena,

Edwin: hebu iweke kwenye simu yako kisha iwashe, cha msingi usiitumie iyo simu kumpigia mtu, sawa kamanda?

Robert: sawa brother!

Edwin: Jitahidi muda wote uwe hewani

Robert: sawa, sawa kaka

Muda si mrefu Robert akaona sms kwenye simu yake

Sms: (dreva to bosi), nimeisha fanya service ya gari bosi soon nitafika kukuchukua

Robert: jamani natoka tutawasiliana

Alichukua koti lake lililokuwa limewekwa kwenye kiti chake na kutoka nje kwa haraka sana mpaka barabarani,

Robert: tax! Tax! hebu nipeleke mtaa wa pili hapo,

Waliondoka kwa kasi mpaka mtaa wa pili walipokuwa umbali wa mita kama kumi hivi kutoka kwenye nyumba ya bosi wakasimama, ilipo toka gari ya bosi wakaanza kuifa kwa nyuma, Robert akiwa kwenye taxi ana watafuta kwa simu rafiki zake Doja na sobba kisha ana wapangia kazi,

Robert: hallo doja

Doja: hallo mkuu nakusikiliza kwa makini nipe mchongo,maana mtaani jua kali sana.

Robert: hope upo jirani na Man sobba, nimekutumia sms inamaelezo yote kabisa

Doja: ndio kaka tumeisha anza kujiandaa

Robert: gwala, nimekutumia na pesa kwenye simu yako, iyo kwaajili ya mahitaji madogomadogo

Doja: sawa mkuu wa kambi,nashukuru kwa kutuweka mjini.

OFISINI – USIKU

Robert anaingia ofisini akiwa kachoka sana, alipoingia tu akaenda moja kwa moja kwenye kiti chake na kujitupa, kisha akashusha pumzi kwa nguvu,

Ian: pole afande

Robert: hahahaha afande wa kanisa huria kachoka sanaa, ila kajaa utajiri wa mahabari makubwa makubwa ya bosi,

Jane: izo taarifa mtapeana wenyewe, hebu sogea hapa unipe taarifa za matumizi yako ya leo niweke kwenye kumbukumbu zangu hapa ili nikalale nimechoka sana,

Robert akasoge nakutoa risiti zote alizo tumia nakukabidhi kwa jane,

Robert: ulikinikabidhi laki 4 nimetumia laki 3 na 20, baadhi ya risiti hizi hapa ila kuna sehemu nilizo kula chakula hawakutoa risiti lakini miamala ya fedha nilizo tuma kwa simu hii hapa pamoja na chenji elfu 80,

Robert akatoa na kumkabidhi simu na fedha za akiba, Jane alipokea na kuweka taarifa zake vizuri huku akionesha kuridhika na maelezo ya Robert,

Robert: nabii Ian kazi imekuwa ngumu lakini yenye mafanikio makubwa sana,

Tulikaa mezan kama dakika 45 hivi tukijadili mambo mbalimbali na nilifanikiwa kuweka mitego yangu na kujiandaa kinabii zaidi.

Umeipenda makala hii? Washirikishe wengine kupitia WhatsApp.

Share WhatsApp

Maoni ya Wasomaji

Maoni yataonekana hapa kama comments zimewashwa kwenye post hii.

Andika Comment